EDUCATION/ NYIRAGONGO
Sous PROVED wa EPST Nyiragongo 1 anaalika viongozi wote wa mashule katika eneo lake kurejesha kwa wazazi pesa walizo lipa ili watoto wao wahudhuriye kwa mitiyani ya serkali wa lwaka wa shule elfu mbili ishirini na tatu-elfu mbili ishirini na ine. Kisuka Baby anajulisha kuwa siku ya mtihani ya tasnifu ama dissertation tarehe sita Mei mwaka huu ndio tarehe ya mwisho ya viongozi wa shule kurudisha pesa hizo. Kada huyu wa sekta ya elimu anaongeza kuwa kuto rudisha pesa hii ni kutoheshimu uamuzi wa serikali. Anajulisha pia kwamba Nyiragongo 1 na 2 zahesabu wanafunzi elfu mbili kati yao mukiwa wahami wa vita mia tano wa somo la mwisho la sekondari. Kisuka Baby anahakikisha kuwa maandalizi yamefanyika ili mitihani hiyo ipitike vizuri na hakuna mwanafunzi atakayekosa mitihani hiyo kwa sababu ni serkali itagaramiya kila mmoja.
Ajouter un commentaire