invité_SW

Soumis par derick le lun 01/04/2024 - 08:38

SECURITE
Shirika nyipya la raia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linamwomba liwali wa kijeshi wa Kivu Kaskazini kuondoa jeshi ndani ya kempbi mbalimbali ya wahami wa vita zinazo kuwa mjini Goma na mazingira yake. Katika barua iliyotumwa kwa kiongozi wa jimbo wiki iliyopita, muundo huu unaonyesha kuwa hesabu visa kadhaa vya vurugu, vitisho na unyanganyii wa bidhaa zinaendeshwa na watu wenye kumiliki silaha waliovalia sare za kijeshi. Prezidenti wa muungano huu anazungumzia kisa cha mauaji kilichorekodiwa huko Lushagala, viwili katika eneo la Rusayo, vingine viwili huko Kanyarutshinya na vitatu huko Bulengo tangu kuanza kwa mwaka huu. BAHIGANA MIRHONYI Germain anaonyesha kuwa zaidi ya visa hivi vya mauaji, muundo wake unaendelea kurekodi aina nyingine za ukiukwaji wa haki za binadamu katika maeneo tofauti. Anatoa wito kwa viongozi wahusika kurejesha usalama katika maeneo ambayo yamekuwa na watu waliokimbia makazi yao kutokana na vita. 

Audio

Ajouter un commentaire

HTML restreint

  • Balises HTML autorisées : <a href hreflang> <em> <strong> <cite> <blockquote cite> <code> <ul type> <ol start type> <li> <dl> <dt> <dd> <h2 id> <h3 id> <h4 id> <h5 id> <h6 id>
  • Les lignes et les paragraphes vont à la ligne automatiquement.
  • Les adresses de pages web et les adresses courriel se transforment en liens automatiquement.